Zingatieni maadili na ueledi wa taaluma yenu wanahabari - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday 11 February 2018

Zingatieni maadili na ueledi wa taaluma yenu wanahabari
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuzingatia maadili na weledi wa taaluma yao katika utendaji kazi ili kukuza taaluma. 

Hayo yamesemwa na mkufunzi wa mafunzo yakuandika habarikwa waandishi wa habari za vijijini BIROSE HAJI MWALIMU yanayoendelea katika Ukumbi wa Wakala Wa Majengo mkoani DODOMA.

Amesemawaandishi wa habari wanatakiwa kutokwenda kinyume na maadili kwa kuandika taarifa za ukweli, pamoja na kutumia vyanzo vinavyoaminika kwa kuzingatia kanuni na taratibu za uandishi wa habari.

Akichangia mada hiyo mmoja wa washiriki katika warsha hiyo MATHIAS TOOKO amesema endapo waandishi wa habari watazingatia waliyofundishwa wataleta ufanisi na kuongeza uaminifu na mvuto kwa wasikilizaji.

Mafunzo hayo ya siku nane yanayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni –UNESCO- yatahitimishwa tarehe 13 mwezi wa pili kwa maadhimisho Siku ya Redio Duniani.

No comments:

Post a Comment