Wamiliki wa vyombo vya habari nchini watakiwa kutoingilia uhuru wa wanahabari katika vituo vyao - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday 11 February 2018

Wamiliki wa vyombo vya habari nchini watakiwa kutoingilia uhuru wa wanahabari katika vituo vyaoWamiliki wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kutoingilia uhuru wa wanahabari katika vituo vyao kwasababu vinaongozwa na sera na misingi yataaluma yahabari.
Hayo yamebainishwa mjini DODOMA na Mkufunzi Mwandamizi wa  Radio za kijamii Bi Rose  Mwalimu katika warsha yakuwajengea uwezo waandishi wa habari vijijini inayowakutanisha wadau wa redio za jamii nchini.
Amesema ni vyema wanahabari wakawa huru katika kutimiza wajibu wao kitaaluma ili kuihudumia jamii na kujiepusha na masuala binafsi.
Warsha hiyo ya siku nane inayo washirikisha wadau wa radio zajamii 24 imeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari kujiendesha kwakujiamini.

No comments:

Post a Comment