Watano wafariki Ajali ya Basi - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 12 February 2018

Watano wafariki Ajali ya Basi
Abiria watano wamekufa papo hapo akiwamo dereva na wengine sita kujeruhiwa baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na gari ndogo katika kitongoji cha Mwituni Kijiji cha Kabuku Mkoani Tanga

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leo Rwegasira, ajali hiyo imetokea leo Februari 12 saa tano.

Kamanda huyo amesema kwamba basi hilo lilikuwa linatokea Lushoto kuelekea Jijini Dar es salaam na na jingine lilitokea Kijiji cha Mkata.

Waliokufa katika ajali hiyo kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Rwegasira  ni dereva wa Hiace, aliyetambulika kwa jina moja la Shaaban huku wengine wanne  wakiwa bado hawajatambuliwa majina yao lakini wote ni wanaume.

“Majeruhi ambao tumewakimbiza hospitali wapo sita akiwamo dereva wa basi kubwa, Khalifa Omar (33) aliyepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na wengine majina yao yatatolewa baada ya madaktari kuwapa huduma ya tiba ya awali,” amesema Rwegasira.

Ali Juma ambaye alishuhudia ajali hiyo na kushiriki uokoaji wa majeruhi amesema alishtuka baada ya kusikia kishindo ndipo aliposogea akaona magari hayo yakiwa yamegongana huku abiria wakiomba kupewa msaada.

Kaimu Kamanda huyo amesema Jeshi la Polisi linafuatilia kujua chanzo cha ajali hiyo na kuwaonya madereva wawapo barabarani kufuata sheria za barabarani.

Chanzo Mwananchi.

No comments:

Post a Comment