Viongozi wa serikali za mitaa na vijiji simameeni upandaji miti wa kila kaya-Kangi - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 21 February 2018

Viongozi wa serikali za mitaa na vijiji simameeni upandaji miti wa kila kaya-Kangi



Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira. mh. Kangi Lugola amewataka wananchi kulima Mazao yanayostahili ukame. 

Kangi Amesema hayo leo katika ziara yake katika wilaya ya Bunda Mkoani Mara kuwa hivi sasa Nchi  zilizoendelea zimezalisha hewa nyingi ya ukaa pamoja na ukataji miti na kupelekea kupoteza Mvua. 

Katika kurejesha uoto wa asili Naibu Waziri ametoa agizo kwa  kila kaya pamoja na shule kupanda miti ikiwa chini ya usimamizi wa viongozi wa serikali za mitaa na vijiji. 

Amesema kila kaya ni lazima ipande miti  mitano (5) Kuanzia sasa .
Kwa upande wa wakulima na wafugaji, ameagiza kuwa ili kulinda ardhi ya mkulima kila mfugaji hataruhusiwa kuchunga kijiji kingine wala shamba la mtu mwingine hata kama shamba hilo halina mazao kwakuwa sio Mali yako.

Amesema mfugaji haruhusiwi kupitisha mifugo kwenye shamba la mwingine. 

Amesema akikamatwa mtu akichunga kwenye shamba la mtu itauzwa na fedha kugawanywa kwa mwenye shamba na serikali ya kijiji husika. 

Mifugo ambayo haitaguswa na fimbo hili ni ile inayoenda kunywa maji au kusafirishwa. 

Hivyo amewaeleza wafugaji wajiandae waamue kuwa na mifugo au kutokuwa nayo. 

Kuhusu uvuvi unaovunja sheria amesema serikali imekataza na lengo ni kuhakikisha samaki wanaongezeka. 

Asema zamani samaki walikuwa wengi  ziwani lakini kwa sasa wameisha kwani watu walikuwa wakienda ziwani wanakuta wanarukaruka kitu ambacho hakipo hivi sasa. 

Amesema kikatiba inawajibu juu wa watu wake kwa kuwa mboga ikikosekana watu hao wataitia misukosuko serikali yao.

Aidha awashukuru wananchi waliotii agizo la serikali ya kuwataka wasalimishe zana haramu za Uvuvi.

No comments:

Post a Comment