wanahabari nchini watakiwa kuzingatia maadili ya taaluma zao. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday 11 February 2018

wanahabari nchini watakiwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.



Waandishi wa habari wa redio za Kijamii nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma zao kwakuandika habari zenye tija kwa jamii .

Wito huo umetolewana Mkufunzi wa Taaluma ya habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO-Bi. ROSE HAJI MWALIMU kwenye mafunzo ya siku nane yanayoendelea  Mjini Dodoma.

Amesema ili jamii inufaike na uwepo wa redio hizo, ni vyema waandishi wa habari  kuzingatia miiko na misingi inayowaongoza  kwa manufaa ya umma.

Kwa upande wao waandishi wa habari wa radio za kijamii wamelishukuru shirika la UNESCO kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasidia  kuboresha utendaji kazi katika vituo vyao. 

Haya ni miongoni mwa mafunzo yanayoendeshwa na Shirika la UNESCO kuzipa uwezo redio za kijamii ili kuandaa habari na vipindi bora.

No comments:

Post a Comment