Nabii aliyewapulizia waumini dawa ya kuua wadudu apatikana na hatia - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday, 10 February 2018

Nabii aliyewapulizia waumini dawa ya kuua wadudu apatikana na hatia

Muhubiri mmoja nchini Afrika Kusini anayejiita 'nabii' anayewapulizia wafuasi wake dawa ya kuua wadudu ,doom, amepatikana na hatia ya unyanyasaji  kulingana na vyombo vya habari.

Lethebo Rabalago, maarufu 'Muhubiri wa doom' alipatikana na hatia ya kukiuka sheria ya kukabiliana na wadudu ,ulisema uamuzi.

Rabalago anadai kwamba dawa hiyo ya wadudu aliyoitumia 2016 inaweza kutibu saratani na virusi vya ugonjwa wa ukimwi.

Hukumu hatahivyo haijatolewa baada ya kutolewa kwa umauzi huo na jaji wa mahakama ya Limpopo.

Siku ya Ijumaa , hakimu Frans Modi alisema kwamba mahakama imempata na hatia na kwamba watu watano waliowasilisha kesi hiyo waliathiriwa kulingana na chombo cha habari cha Afrika Kusini SABC.

Hakimu huyo alisema, hatua ya kuwapulizia dawa hiyo walalamishi katika nyuso zao inafanya kosa hilo kuwa baya zaidi.

Pia alifichua kwamba baadhi yao walikuwa wamepata athari mbaya kama vile kikohozi zaidi ya miezi saba baada ya kisa hicho.

Rabalago ambaye anasimamia kanisa la Mount Zion General Assembly alikamatwa baada ya kubainika kwamba alitumia dawa hiyo kuwatibu wafuasi wake magonjwa kadhaa 2016.

Katika picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii alionekana akiwapulizia dawa hiyo ya wadudu katika macho yao mbali na sehemu nyengine mwilini.


Wakati huo aliambia mwandishi wa habari wa BBC Nomsa Maseko mjini Johannesburg kwamba alimpulizia usoni mwanamke mmoja kwa sababu alikuwa na ugonjwa wa macho na kusema kuwa mwanamke huyo alipona kwasababu aliamini uwezo wa Mungu.

No comments:

Post a Comment