MWENYEKITI wa kamati ya Watoto Katika kompasheni Kanisa la ANGILKAN Mjini Bunda
Mkoani Mara Bwana FLAVIAN JOSEPH NYAMIGEKO amesema huduma zanazitolewa na
kompashen hiyo imesaidia kupunguza wimbi la watoto wa mitaani mjini halo.
Amesema Katika Kanisa lao la ANGILKAN kupitia kompashen hiyo inalea
jumla ya watoto 296 wanaolewa mahitaji yote muhimu za kibinadamu.
Bwana Flavian ameeleza kuwa pamoja na kuepusha madhila ya uwepo wa
watoto wa mitaani lakini wao jukumu lao ni kuwasimamia watoto hao hadi pale
watakapo jimudu kimaisha.
Ameeleza huduma wanazopewa watoto hao ni pamoja na kuwasomesha,
kuwapatia huduma ya afya pindi wanapougua pamoja na kuwapatia nyenzo za
kuendeshea Maisha wawapo katika hatua za kujitegemea.
Hata hivyo amewaomba wananchi kuwathamini watoto wanaishi Katika
mazingira magumu kwani wao ni watu na wanapaswa kupatiwa huduma kama watu
wengine na kuongeza kuwa katika mtihani wa kidato cha nne yaliyotolewa matokeo
hivi karibuni jumla ya watoto 28 wamefaulu wanaosimamiwa na Compashen.
No comments:
Post a Comment