Serikali yatoa agizo walimu wa sekondari - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 20 February 2018

Serikali yatoa agizo walimu wa sekondariSerikali imesema mwalimu wa sekondari kufundisha shule ya msingi si kushushwa cheo na wala si jambo la ajabu.

Taarifa ya mkuu wa kitengo cha mawasiliano Ofisi ya Rais (Utumishi), Florence Lawrence imesema Serikali kuwapangia baadhi ya walimu wa sekondari kufundisha shule za msingi ni moja ya hatua za kuongeza ufanisi na kuleta mgawanyo sawa wa walimu katika shule hizo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro amekaririwa katika taarifa hiyo iliyotolewa leo Februari 20,2018 akisema hatua hiyo haimaanishi kuwa walimu wanaotoka katika shule ya sekondari kwenda kufundisha msingi wameshushwa cheo.

Dk Ndumbaro ametoa ufafanuzi huo katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako.

Amesema lengo la Serikali ni kuondoa upungufu wa walimu katika shule za msingi na kuimarisha utoaji wa elimu.

Katibu mkuu ameainisha kuwa sifa za kufundisha na kiwango cha elimu zinaendana na mabadiliko yanayotokea duniani, hivyo mwalimu mwenye elimu ya kiwango cha Shahada ya kwanza kufundisha shule ya msingi isionekane ni jambo la ajabu.

Dk Ndumbaro amewaambia watumishi wa umma kuwa, maendeleo katika sekta yoyote, ikiwamo ya elimu yanakuja na mabadiliko hivyo wayapokee na kufanya kazi ili kufikia lengo.

No comments:

Post a Comment