Umoja
vijana wa chama cha mapinduzi uvccm wilaya ya Bunda mkoani Mara chini ya
mwenyekiti wake gasper Charles wameshiriki kutoa msaada wa kusaidia ujenzi katika
kituo cha afya bunda kinacho jengwa katika kata ya Kabarimu.
Akizungumza
na vyombo vya habari katika eneo la ujenzi wa kituo hicho cha afya Bwana Gasper
amesema kuwa katika kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi wameamu kuungana na
viongozi wa chama hicho katika ujenzi huo kwa maslahi mapana ya wananchi pamoja
na kumsaidia rais john pombe magufuli kusimamia miradi ya maendeleo
inayoendelea nchini.
Naye
katibu wa umoja huo shija steven amewaomba vijana mjini bunda kutumia miradi ya
maendeleo inayotekelezwa na serikali kujipatia ajira badala ya kukaa vijiweni
bila kazi.
Hata
hivyo katika kusaidia ujenzi wa kituo hicho mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wilaya ya Bunda ambae pia ni mkuu wa wilaya Mwl. Lydia Bupilipili ameshirikiana na vijana hao
katika kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho kilichotolewa fhedha shilingimilioni
mia tano inakamilika kwa ufanisi wa hali ya juu , pia amewapongeza vijana wa
umoja wa chama hicho katika kuonyesha uzalendo wa kweli.
No comments:
Post a Comment