Wananchi katika kata ya
Balili halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara Wameiomba serikali kuwakubalia
wananchi kuwaadhibu wahalifu.
Akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara katani hapo Petro Nyamagaka mkazi wa eneo hilo amedai kuwa
anashangazwa na hatua ya jeshi la polisi kuwazuia wananchi kumuadhibu mwizi
kwani ilhali anapofikishwa kituo cha polisi badae huachwa huru.
Amesema kitendo cha
kuaachia huru huongeza hofu kwa wananchi na wakati mwingine huwapa nguvu
wahalifu kuendelea na vitendo viovu katika jamii.
Kwa upande wake afisa
polisi kata amewahakikishia wakazi wa mtaa wa rubana na kata ya balili kiujumla
kwamba mhalifu akifikishwa jeshi la polisi na wananchi wakatoa ushahidi hatua
za kisheria hutekeleza kama kawaida.
Aidha ameeleza kwamba changamoto
inayosababisha wahalifu hao wanaachwa ni pale ushaidi unapokosekana, na
kuwasihi wananchi kutoa ushirikiano pindi wanapotakiwa kufanya hivyo ili haki
itendeke.
Naye Mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama ambae pia ni Mtendaji wa kata hiyo Bwana Thomas
Bure amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola katika masuala ya
ulinzi na usalama ili kupunguza vitendo viovu katika maeneo yao.
Amesema wakati huu
ambapo wananchi wengi wamelima zao la pamba na wanategemea kupata pesa nyingi
nidhahiri kuwa wezi wataongezeka kwahiyo wanatakiwa kuunda vikundi vya ulinzi
vitakavyosaidia kudhibiti wizi na uporajimdogomdogo.
Bwana Bure ameeleza
kwamba wakati watakapounda hivyo vikundi jeshi la polisi litawapatia mafunzo ya
namna bora ya kukamata wahalifu .
Hata hivyo ametoa wito
kwa wakazi hao kufuata sheria badala ya kujichukulia sheria mkononi kwakuwa
kufanya hivyo ni kwenda kinyume na utaratibu wa nchi na atakayefanya hivyo
hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment