Wananchi wilayani Bunda toeni ushirikiano kwa watafiti-Adam Malima - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 19 February 2018

Wananchi wilayani Bunda toeni ushirikiano kwa watafiti-Adam Malima


SERIKALI  mkoani Mara imewataka  wananchi kutoa ushirikiano  kwa watafiti  wakati wa utafiti wa Mapato na na matumizi ya kaya  binafsi Tanzania bara wa mwaka 2017/2018 unaoendelea nchini hivi sasa.
Mkuu wa mkoa Mara, Adam Malima alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi  wa habari ofisini kwake ambap[o alisema  utafiti umeanza  na unaendelea  ndani ya mkoa wa Mara.

Alisema Utafiti huo wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania bara unatarajia kukusanya taarifa kutoka katika kaya binafsi katika Nyanja mbalimbali  ikiwa ni pamoja  wanakaya, uzazi  na unyonyeshaji.

“Lakini pia utafiti huu wa kaya binafsi utahusisha elimu, afya, uraia, uhamiaji, ulemavu, Bima, hali ya ajira, biashara na mapato  ya kaya na makazi ya kaya” alisema Malimu. 

Taarifa zingine zitakazokusanywa ni  matumizi na nishati, huduma za maji safi, na maji taka, utalii wa ndani, uwekezaji wa kaya, matumizi ya huduma za kifedha , upatikanaji wa usalama wa chakula, matumizi, mazingira  na  umiliki wa vitambulisho mbalimbali.

Utafiti utajumuisha pia kilimo na mifugo, matumizi ya muda kwa kila mwanakay mwenye umri wa miaka 5 kuendelea, mapato na matumizi ya kila kaya na mawanakaya.

Malima  alifafanua kuwa Ofisi ya taifa ya Takwimu ni taasisi inayofanya kazi zake kwa mujibu wa sheria mpya ya takwimu ya mwaka 2015 ambapo wa mujibu wa sheria kifungu cha 37(3)kinataka ushiriki wa wananchi katika utafiti mbalimbali zinazokusanywa na serikali.


Alisema kwa mujibu  wa sheria ya takwimu namba 9 ya mwaka 2015  taarifa zinazokusanywa kutoka kila kaya pamoja na wanakaya zitatunzwa kwa usiri mkubwa kama inavyotakiwa.

Aidha mkuu wa mkoa huyo alitaja baadhi ya maeneo  yatakayohusishwa  na utafiti kama sampuli mkoani humo ni kiongera, Nyarero,Kenyamosabi,  Magoma, Nyangoto, Kitenga na Nyabitocho katika wilaya ya Tarime.

Wilaya ya Serengeti ni Kijiji  cha Nyiboko,Natta mbiso, Nyanungu, Mbirikili, na Bomani ambapo wilaya ya Musoma vijijini ni Bugunda, Muhoji, Bwai Kumsoma na Kigeraetuma.

Alitaja Vijiji katika wilaya ya Bunda kuwa utafiti utahusisha Manchimweru, Serengeti, Kigaga, Karukekere, Nyamakokoto na Balili, wakati  katika Manispaa ya Musoma ni Nyasho Magereza, Mlimani, Mkinyerero, wilaya ya Rorya ni kijiji cha Rwang’enyi, Kyariko, Sakawa, Nyanduga na Kwibuse.

Katika Wilaya ya Butiama utafiti utakuwa katika vijiji vya Masurura, Mirwa, Kyatungwe na Busirime na kwamba kwa kila kaya  watahojiwa kwa muda wa siku 14..

No comments:

Post a Comment