Chadema yamjia juu msimamizi wa uchaguzi - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 12 February 2018

Chadema yamjia juu msimamizi wa uchaguzi



Chadema imemlalamikia msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni ikidai anaashiria kuharibu uchaguzi wa Februari 17,2018.

Chama hicho kimedai kutowapa viapo mawakala juzi Februari 10,2018 kunaashiria njama za kutaka wasishiriki shughuli za upigaji na kuhesabu kura.

Viongozi wa Chadema wamesema hayo jana Februari 11,2018 walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi  mdogo katika jimbo hilo na la Siha pamoja na kata tisa.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema sheria inataka mawakala wa upigaji kura kula kiapo cha kutunza siri siku saba kabla ya kupiga kura na wanapaswa kupewa kiapo hicho.

"Anayeapisha ndiye anayesaini, hawezi kuapa mbele ya mtu mmoja na kusaini mwingine, kwa kila mwapishaji katika kila kata anakuwa na sababu zake, msimamizi wa uchaguzi anatumika," alidai Kigaila.

Kigaila alisema, "Kinachoendelea Kinondoni ni tofauti na Siha, kule Siha wameapa jana na kila wakala ameondoka na kiapo chake, sasa sijui sheria inayotumika Siha ni tofauti na inayotumika Kinondoni. "

Meneja kampeni wa Chadema Kinondoni, Saed Kubenea alisema kila linalopangwa kutaka kuuharibu uchaguzi huo hawatalikubali.

No comments:

Post a Comment