Kituo cha Radio mazingira fm kimepongezwa kwa kuibua na kuripoti matatizo mbalimbali ndani ya jamii. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 14 February 2018

Kituo cha Radio mazingira fm kimepongezwa kwa kuibua na kuripoti matatizo mbalimbali ndani ya jamii.Kituo cha Radio mazingira fm kimepongezwa kwa kuibua na kuripoti matatizo mbalimbali ndani ya jamii. 

Pongezi hizo zimetolewa na Afisa ustawi wa jamii halmashauri ya mji wa Bunda Pius Masalu kupitia kipindi cha Duru za habari jioni leo huku Akitolea mfano wa tukio la mama mmoja aliyetelekeza watoto wawili mmoja akiwa ni mtoto wake na mwingine akiwa ni mjukuu wake katika mtaa wa Majengo kata ya nyasura ambapo amesema amepata taarifa ya tukio hilo kupitia radio Mazingira fm.

Sambamba na hilo pia amesema kuwa kazi inayofanywa na radio mazingira ni jambo la kujivunia katika Halmashauri ya mji wa Bunda na hata Mkoa wa mara na maeneo jirani inakofika ambapo 91.7 Mazingira akisema kuwa imekuwa ni msaada mkubwa kwa jamii kutokana wanafanyakazi wake kutokuchoka kufika ndani ya jamii na kuibua na kuripoti matatizo mbalmbali.

Hata hivyo ametoa wito kwa uongozi na timu mzima ya kituo cha radio kuendelea na kasi hiyo ili jamii iendelee kunufaika na uwepo wao ndani ya jamii.

No comments:

Post a Comment