Mfaransa wa simba ataka mwendo na mabao kuwamaliza gendamarie leo. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday 11 February 2018

Mfaransa wa simba ataka mwendo na mabao kuwamaliza gendamarie leo.Kikosi cha Simba kitashambulia mfululizo na kwa kasi kubwa katika mechi yao dhidi ya Gendamarie kutoka Djibouti.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza, Kocha Mkuu, Pierre Lechantre amewataka wachezaji wake kucheza kwa kasi na kushambulia mfulilizo ili kupata mabao ya haraka.

Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika, inapigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Kocha anataka kushambulia na kupata mabao, amewaeleza wachezaji mengi lakini kikubwa ni umakini katika umaliziaji,” kilieleza chanzo.

Kocha huyo alikaa na wachezaji wake na kutumia zaidi ya nusu saa akiwaeleza kinachotakiwa kufanyika katika mechi hiyo ya Gendamarie ambao wanaonekana ni dhaifu.


Hata hivyo, kocha huyo inaelezwa amewasisitiza kutotanguliza dharau na kuhakikisha wanashinda kwa mabao idadi nzuri.

No comments:

Post a Comment