Serikali haiogopi mtu katika suala la uvuvi haramu-Bupilipili - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 12 February 2018

Serikali haiogopi mtu katika suala la uvuvi haramu-Bupilipili



Mkuu wa wilaya ya Bunda Mkoani Mara Mwl.Lydia Bupilipili  ametoa onyo kwa wale wanaotumika kukwamisha suala la kutokomeza uvuvi haramu ndani ya wilaya ya Bunda kwa  kufuata mkumbo bila kujuwa kuwa kile wanachokifanya ni kinyume cha sheria.

Bupilipili ametoa onyo hilo leo wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake kuhusu utoaji wa taarifa kwa umma hatua waliyofikia katika mapambano hayo ya uvuvi haramu.

Bupilipili amesema kwa kushirikiana na ofisi ya uvuvi wanaendelea kufanya kazi ya kuhakikisha wanawashughulikia wale wote wanaojihusisha na shughuli hiyo ya uvuvi haramu wanaacha mara moja.

Bupilipili amesema serikali haimuogopi mtu yeyote hivyo wale wanaojidanganya kuwa wanawaogopa wafute mawazo hayo na wajuwe kuwa wanashughulikiwa kwa mujibu na wa sheria za nchi na si vinginevyo.

Katika hatua nyingine Bupilipili amesema kesho February 13 2018  watafanya usaili wa vijana wa mgambo waliotuma maombi yao ya kazi ya kujiunga na kazi ya  ulinzi Suma JKT ambapo usaili utaanza saa mbili kamili asubuhi.






No comments:

Post a Comment