Wakili wa Haki za Binadamu afikishwa Mahakamani Kenya - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 12 February 2018

Wakili wa Haki za Binadamu afikishwa Mahakamani Kenya
Moja ya habari zilizotufikia kutoka nchini Kenya ni pamoja na inayomhusu Wakili maarufu wa Haki za Binadamu Haron Ndubi ambaye amefikishwa Mahakamani asubuhi ya leo February 12, 2018.

Wakili Ndubi amefikishwa Mahakamani baada ya kubishana na Maaskari wa barabarani baada ya kukataa kufuata maelekezo aliyopewa na askari hao, tukio ambalo limetokea katika Barabara ya Jakaya Kikwete.

Inaelezwa kuwa Maaskari hao walimwagiza kupumua kwenye kifaa maalumu cha kupima dereva ana kiwango gani cha pombe mwilini kutokana na kuhisi kuwa Wakili huyo alikuwa akiendesha gari akiwa amelewa.

Hata hivyo ameachiwa kwa dhamana ya Ksh 30000 sawa na Tshs 67000.

No comments:

Post a Comment