Wananchi katika kijiji cha Bitaraguru kata ya Kabasa Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara wameiomba serikali iwefungulie zahanati ya bitaraguru ambayo kwa sasa haitoi huduma kwa wananchi licha ya kuonekana kukamilika.
Ombi hilo
limetolewa na wananchi hao kupitia kipindi cha Duru za Habari kinachorushwa na
kituo hiki baada ya kufika eneo hilo kuzungumza na wananchi kuhusu maoni yao
jinsi walivyopokea mradi huo mkubwa ambao unaonekana kukamilika.
IMELDA BWIRE pamoja na LETICIA JOSEPHAT wamesema kuwa ni muda sasa hawaoni zahanati hiyo inaanza kutoa huduma
licha ya wao kuona imekamilika.
Aidha
wamesema watafurahi sana siku ambayo
zahanati hiyo itaanza kutoa huduma kwa wananchi kwani itakuwa imewasaidia
sehemu kubwa katika shida walizokuwa wanazipata kama wananchi wa eneo hilo.
Naye PAULO KASERA ambaye ni mmoja ya
viongozi kutoka kijiji hicho amesema kuwa serikali ya kijiji inafuatilia
kuuliza kuhusu kufunguliwa kwa zahanati hiyo wanaambiwa kuwa zahanati hiyo
haijafikia kufunguliwa maana bado haijasajiliwa.
Katika juhudi
za kumtafuta mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Bunda ili kupata ufafanuzi wa
suala hilo bado zinaendelea.
No comments:
Post a Comment