Manchester United wakutwa na msiba - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 10 February 2018

Manchester United wakutwa na msiba

Simanzi kubwa imetapakaa katika jiji la Cork Nchini Ireland baada ya aliyekuwa mchezaji Nguli wa Timu ya taifa na klabu za Celtic, Sunderland na Man United kupoteza maisha kwa ugonjwa wa saratani. Raisi wa Ireland Mapema hivi leo ametoa salamu za rambirambi kwa ndugu na familia yote ya michezo kwa kumpoteza Liam Miller aliyefariki dunia akiwa na umri miaka 36.
Liam Miller alianzia maisha yake ya soka katika Klabu ya Celtic mwaka 2000. Baadae alijiunga Na Man United Mnamo mwaka 2004 na aliichezea michezo 9 tu kabla ya kwenda kwa mkopo Leeds United.
Mnamo mwezi wa 11 mwaka jana familia yake ilitangaza Miller anasumbuliwa na Matatizo ya tumbo na baadae ilijulikana kuwa ni Kansa. Miller ameacha watoto wawili wa kiume na mtoto mmoja wa kike na mjane ajulikanae kama Clare.
Kocha wake wa Zamani Bwana John Hughes aliyefanya nae kazi katika klabu ya Hebirnian amemtaja Miller kama mchezaji aliyekamilika aliyewahi kumfundisha. Anasema kuwa liam alikuwa anatangulia kwenye kiwanja cha mazoezi dakika 15 kabla ya mazoezi. Na alikuwa akipenda sana kufanya mazoezi na vijana wadogo na watoto.
Liam alibahatika kuzichezea klabu 12 katika maisha yake ya Soka. Alifunga magoli 19 katika michezo 346. Ametwaa kombe la ligi ku Scotland, na kombe la ligi daraja la kwanza England, pia ametwa kombe la Eufa la wachezaji wa umri wa miaka 16 akiwa naa timu ya taifa.
Pia ni msomi alisoma katika chuo cha Ciachford. Aliwahi kuwasifia Kocha mkuu wa United Sir alex Ferguson na Martin Onel kwa kuwa watu walioinua kipaji chake.

No comments:

Post a Comment