Waandishi wa Habari Redio za Kijamii Tanzania watakiwa kutumia fursa zinazotolewa na Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni –UNESCO - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday 11 February 2018

Waandishi wa Habari Redio za Kijamii Tanzania watakiwa kutumia fursa zinazotolewa na Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni –UNESCO



Waandishi wa Habari kutoka Redio za Kijamii  Tanzania wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni –UNESCO-ili kuleta mabadiliko kwa Jamii.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Jamii Tanzania –TADIO -,PROSPER KWIGIZE  katika mafunzo yanayoendelea mjini DODOMA,yanayo shirikisha waandishi wahabari 49 kutoka redio 24 zajamii. 

Bwana KWIGIZE amesema mafunzo kwa waandishi wahabari hususani katika maeneo yamazingira na jinsia hutolewa kwakulipia kiasi cha ada lakini UNESCO hutoa mafunzo kama hayo bila malipo yoyote.

Amesema ni vyema kuthamini na kuzingatia elimu wanayoipata waandishi katika mtandao wa TADIO na kuifanyia kazi kwa manufaa ya jamii.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo ROSE HAJI MWALIMU ametoa wito kwa waandishi wa habari kutoka redio za kijamii kuibua changamoto zinazochangia kuleta usawa katika masuala ya kijinsia.

No comments:

Post a Comment