CCM Bunda yamkataa DC wa wilaya hiyo, wamuomba rais Magufuli amhamishie wilaya nyingine - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 10 February 2018

CCM Bunda yamkataa DC wa wilaya hiyo, wamuomba rais Magufuli amhamishie wilaya nyingineHalmashauri kuu Chama cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Bunda mkoani Mara, kimepitisha azimio la kumkataa mkuu wa wilaya hiyo, na kumuomba Rais Dk. John Magufuli kumhamisha, kwani atasababisisha maendeleo katika wilaya hiyo kukwama.

Azimio hilo limefikiwa baada ya kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho kukaa jana ikiwa ni sehemu ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kuanzia July 2017 hadi December 2017.

Hata hivyo kimekataa kupokea taarifa ya mkuu huyo wa wilaya  ya utekelezaji wa ilani ya CCM aliyokuwa anaiwasilisha ambapo wamedai kuwa ina mapungufu mengi.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa CCM mkoani Mara, Samweli Kiboye maarufu kwa jina la namba tatu, amesema mkuu wa wilaya ya Bunda, pamoja na mkuu wa wilaya ya Tarime ni mzigo kwa chama hicho.

No comments:

Post a Comment