Friday, 23 March 2018

Tafuteni suluhu ya pamoja ili kuzuia wanyama pori waharibifu mashambani-Bunda Mara



Wakazi  wa  vijiji   vinavyopakana  na hifadhi ya taifa ya Serengeti  wamehamasishwa kutafuta suluhu ya pamoja ili kuzuia wanyama pori waharibifu ambao wamekuwa changamoto katika vijiji vyao.

Akizungumza  na  wananchi  wa kijiji  cha Tingirima kilichopo kata ya Mugeta wilayani  Bunda mwakilishi kutoka kampuni ya wawekezaji  ya Grumet Fund David Mwakipesile  ambao  pia ni waratibu  wa elimu hiyo  amesema kuwa kama kampuni wameamua kutoa elimu hiyo kwa vijiji vyote vya wilaya ya Bunda hasa vijiji vya Mugeta, kyandege, sarakwa,mariwanda,kihumbu,hunyari, nyamatoke,bukhore, kunzugu na kumaliza na kijiji cha balili kwa kusudi la kuweka mikakati ya pamoja ya kuzuia wanyama pori waharibifu.

Mwakipesile  amewaambia  wanaTingirima kuwa wao kama kampuni baada ya kuona tatizo la wanyama  waharibifu kama tatizo la kitaifa wameamua kuanzisha kikosi maalum kinachosaidia kufukuza wanyama hao na kuwataka wananchi  kutoa ushirikiano kwa kikosi hicho .

Naye afisa Wanyama pori wilaya ya Bunda Marwa Kitende  amesema kuwa lengo la serikali siyo kulipa fidia ama kifuta machozi  kwa wananchi  bali lengo lao ni kuhakikisha wanazuia wanyama hao kabla hawajafanya uharibifu.

Soma Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 23



Wednesday, 21 March 2018

Jeshi la polisi la kanusha kusababisha ajali ya mwanafunzi wa darasa la pili -Bunda Mara

Wanafunzi katika shule ya msingi Balili B halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara wameandamana mapema leo  asubuhi hadi zilipo ofisi ya mkurugenzi wa mji baada ya mwenzao kugongwa kwa gari  na kupelekea kifo chake katika kivuko cha watembea kwa miguu kilichopo karibu na shule hiyo.

Tukio hilo la kugongwa kwa gari hadi kufa limempata Mwanafunzi  wa darasa la sita aitwae Julius Nyerere mwenye umri wa miaka 12 na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali teuli ya wilaya ya Bunda DDH.

Mashuhuda wa Tukio hilo wamesema wameshuhudia mwanafunzi huyo akigongwa  kwa gari lenye rangi ya Dark blue ambalo wao wamelihusisha na gari la askari mmoja wa jeshi la polisi.
Kufuatia tukio hilo mwalimu flora isack anaefundisha katika shule hiyo amewalalamikia baadhi ya askari wa jeshi la polisi kumpiga na kumdhalilisha kwa kumvua nguo kwa kile alichoeleza kwamba alihusika kuhamasisha wanafunzi kufunga barabara na kuponda kwa mawe baadhi ya magari ya abiria yaliyokuwa yakipita kuelekea mwanza na musoma.
Kwa upende wa jeshi la polisi wilaya ya Bunda kupitia kwa OCD Jeremia Shila amekiri kutokea kwa tukio hilo la mwanafunzi kugongwa kwa gari hadi kufa ambapo amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na ufuatiliaji wa gari lililohusika na ajili hiyo.
Kwa upande wa madai ya askari wa polisi kuhusishwa na ajali hiyo pamoja na kumshambulia mwali huyo kamanda shila amepinga taarifa hizo na kueleza kuwa tukio hilo limesababishwa na kijana mmoja ambae baadae gari lake lililohusika na ajali limeonekana musoma na wanaendelea kulifuatilia ambapo ameaidi kutoa taarifa kwa umma pindi watakapokamilisha utaratibu wa kumkamata mhusika.

Aidha kuhusu mwalimu flora kushambuliwa amesame hakushambuliwa badala yake alikuwa akiondolewa barabarani kupisha watumiaji wengine wa barabara kuendelea na shughuli zao.

Monday, 19 March 2018

Wake za Marehemu Wafichua Mazito, Kifo cha Mmiliki wa Super Sami

                      

Mapya yameibuka kufuatia kifo cha mfanyabiashara mabye ni tajiri wa mabasi ya kampuni ya Super Sami, Samson Josiah almaarufu Super Sami, mkazi wa Magu Mwanza, baada ya wake zake kufunguka na kueleza ya moyoni kuhusu tukio hilo la kusikitisha huku mkewe mdogo akimfichua anayemhisi kuwa muuaji.

Mfanyabiashara huyo alipotea katika mazingira ya kutatanisha kwa siku kadhaa kabla ya mwili wake kuonekana katika mto Ndabaka, wilayani Bunda Mkoani Mara ukiwa umefungwa kwenye kiroba na kuharibika vibaya. 

Kwa nyakati tofauti wake wa marehemu walizungumza na Ijumaa Wikienda na kutoa maoni yao, huku wakieleza mambo wanayoamini kuwa yanaweza kuchangia kifo cha mume wao.

Mange kimambi aibukia tarime.


Mbunge wa Serengeti,mkoani Mara Marwa Ryoba Chacha (CHADEMA) ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha polisi kutaka kuzuia mkutano wa Mbunge wa Tarime Vijijini CHADEMA, Mhe. John Heche kwa kile kinachodaiwa kuhofia maandamano yanayoratibiwa na Mange Kimambi.

Marwa Ryoba amesema kuwa polisi wamekuwa na upendeleo kwa kuwa wanaona watu wa CCM wakiendelea kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa ili hali watu wa upinzani wakizuiliwa. 

"Haki huinua taifa; bali dhambi ni aibu ya watu wote. Nimepata taarifa kwamba Mbunge wa Tarime vijijini Mh. John Heche alizuiliwa asifanye mkutano Sirari eti kisa kuna maandamano ya Mange Kimambi, kwanza maandamano sio dhambi yapo kwa mujibu wa katiba yetu" ,alisema Mbunge Marwa Ryoba 

Kwa mujibu wa Mbunge wa Tarime Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA, John Heche amethibitisha hilo kuwa ni kweli kulikuwa na jaribio la kutaka kuzuiwa kufanya mkutano wake na wananchi wa Sirari kwa hofu ya maandamano ya tarehe 26 mwezi wa nne. 

"Ni kweli polisi walitaka kutuzuia kufanya mkutano ila pamoja na polisi Sirari kufanya jaribio la kutaka kuzuia mkutano wangu na wananchi, kwa kisingizio cha hofu ya maandamano ya tarehe 26. Mkutano wangu ulifanyika na umemalizika salama, Asanteni sana wananchi wa Sirari kwa kujitokeza kwenye mkutano wetu" alisema John Heche.