Hii ni moja ya picha ya
choo ya shule hiyo
Shule ya
Msingi Kilimani iliyopo kata ya Nyasura Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara huenda ikafungwa kufuatia
Kamati ya shule hiyo kumuandikia mhutasari Mkurungezi mtendaji wa Halmashauri
ya mji wa Bunda Janeth Mayanja wakiomba kufungiwa shule yao kwani choo ya shule
hiyo imejaa choo na kupelekea wanafunzi
shule hiyo kujisaidia nje ya jengo la choo na kwenye mashamba ambayo yapo
karibu na eneo la shule hiyo.
Akizungumza
na Radio Mazingira fm mapema leo Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Kyinza Juma
amesema wamefikia maamuzi hayo baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya katika
shule hiyo hivyo wameona kunyamaza kimya
sio suluhu ya jambo hilo.
Juma amesema
asaivi ni musimu wa mvua hivyo wasipochukuwa hatua za haraka asaivi inaweza
kuleta madhara makubwa kwa wanafunzi hao kwani choo hicho kimejaa na kwamba inafikia hatua hadi funza
wanaonekana juu katika matundu ya choo hicho.
Aidha Juma
amesema siku ya leo Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwl.Lydia Bupilipili amefika katika
shule hiyo na kujionea hali ilivyo huku akisema hakuwa na taarifa kuhusiana na
changamoto hiyo hivyo amepata taarifa kupitia Radio mazingira fm ndio akaamua
kufatilia suala hilo.
Hata hivyo
baada ya Mkuu wa wilaya ya Bunda mwl.Lydia Bupilipili kupata taarifa hizi
kupitia kituo hiki ameamua kufuatilia suala hilo na kusema kuwa ni kweli
amejionea hali hiyo na kwamba tayari ameshazungumza na Mkurungezi wa
Halmashauri ya mji wa Bunda na hatua zimeanza kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment