BREAKING NEWS: Tume ya Haki za Binadamu Yafungukia Matukio ya Uchaguzi - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 1 March 2018

BREAKING NEWS: Tume ya Haki za Binadamu Yafungukia Matukio ya Uchaguzi

Tume ya Haki za Binadamu Yafungukia Matukio ya Uchaguzi Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetoa taarifa kwa umma kuhusu tathimini juu ya matukio yaliyotokea katika kipindi cha uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, na Siha mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi msaidizi wa kituo hicho, Anna Henga, amesema katika kipindi cha kampeni waliona matumizi ya watoto katika kampeni, na kushuhudia video ya mtoto akinengua na kutumbuiza jukwaani katika kampeni za chama cha mapinduzi (CCM), kitu ambacho ni ukiukwaji mkubwa sana wa haki za binadamu hususani kwa watoto.

 Pia kituo hicho kilishuhudia matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya vyama, kitendo ambacho kilifanywa na CCM katika jimbo la Siha kumnadi mgombea wao Dkt Mollel.

Aidha kituo hicho kimebainisha kuwa kiliona matumizi ya nguvu katika kipindi cha kampeni yaliyopelekea raia kuumizwa na kusababisha kifo cha mwanafunzi wa (NIT), Akwilina Akwilini, Februari 16, kilichosababishwa na jeshi la polisi walipokuwa wakidhibiti maaandamano ya Chadema, na kuwashikilia raia 40.

Na Katika siku ya kupiga kura, kituo hicho kimeshuhudia mwitikio mdogo wa wapiga kura, unyanyasaji wa mawakala wa vyama vya siasa kwa kutopewa kwa wakati viapo.

No comments:

Post a Comment