Sauti ya Jamii — redio yenye maudhui ya kijamii kutoka Bunda, Mkoa wa Mara.
Wasifu wa Kituo
Mazingira FM ni kituo cha redio chenye maudhui ya kijamii kilichoanzishwa mwaka 2011. Kituo kinarusha matangazo yake kutoka Bunda, Mkoa wa Mara, na kusikika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani, ikiwemo Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza kama Magu na Ukerewe.
Kupitia vipindi na matangazo yake, Mazingira FM hutoa habari, elimu, mazingira, afya, michezo na burudani kwa jamii.
MTANDAO WETU
Vituo Vinne vya Matangazo
BUNDAKituo Kikuu
MUSOMAMara
TARIMEMara
MUGUMU–SERENGETIMara
SAUTI YA JAMII
Redio ya Jamii
Mazingira FM inalenga kuipa jamii nafasi ya kupata habari na maarifa, kusikiliza mijadala yenye manufaa, kushiriki katika masuala yanayoigusa na kupata burudani kupitia vipindi vinavyoakisi maisha ya jamii.
Mazingira FM ni kituo cha redio chenye maudhui ya kijamii kilichoanzishwa mwaka 2011. Kituo kinarusha matangazo yake kutoka Bunda, Mkoa wa Mara, na kusikika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani, ikiwemo Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza kama Magu na Ukerewe. Kupitia vipindi na matangazo yake, Mazingira FM hutoa habari, elimu, mazingira, afya, michezo na burudani kwa jamii.
HABARI ZAIDIHabari kutoka kwenye kumbukumbu za Mazingira FM
Tuesday, 6 March 2018
NABII MTOTO TAJIRI: Anayegawa Pesa, Anaponyesha Ukimwi..!
KILA kukicha
wanatokea manabii wanaokuja na staili mbalimbali za mahubiri na miujiza ya kila
aina, wakati Nabii Tito ambaye alikuwa akihubiri mitaani kwamba kuzini na
kulewa siyo dhambi, akisota Hospitali ya Mirembe mkoni Dodoma, baada ya
kuonekana kwamba ana matatizo ya akili, mwingine aliyetambulika kwa jina la
Daniel Daniel Shilla (22), ameibuka na kutikisa Jiji la Dar. Nabii huyo mtoto
ambaye ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kugawa pesa kwa waumini
wanaosali kanisani kwake, anaongoza kanisa linalojulikana kwa jina la Bethel
International Ministry Of Tanzania, lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba na
Kigamboni kwa jijini Dar na matawi mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Zanzibar,
Kigoma, Morogoro na mengineyo.
Baada ya kuwepo kwa tuhuma nzito za kuwa na
utajiri mkubwa usiokuwa na vielelezo, kuusishwa na Freemasons na masuala ya
utapeli kwa wanaohitaji huduma zake za maombezi, Ijumaa Wikienda liliamua
kumsaka Nabii Shilla na kukuletea stori kamili.
No comments:
Post a Comment