Wafanyabiashara Nyasura waomba waboreshewe soko kabla ya kuhamishwa.Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 15 March 2018

Wafanyabiashara Nyasura waomba waboreshewe soko kabla ya kuhamishwa.Bunda Mara
                           Picha ya muonekano wa soko hilo
Wafanyabiashara ndogondogo katika genge la Nyasura kata ya Nyasura Halmashauri ya mji wa Bunda mkoa wa Mara  wamesema kama serikali ya Halmashauri ya mji wa Bunda inataka iwahamishie katika soko la manjembe basi ni vizuri hata mnada na stand ya magari ikaanzishwa huko ili kuleta chachu ya biashara katika eneo hilo.

Wafanyabiashara hao Wametoa  ombi hilo leo wakati wakizungumza na mazingira fm katika genge la Nyasura ambapo wamesema kuwa wao hawajakataa na hawapingani na serikali kuhusu kuhama bali serikali iwaboreshee mazingira ya soko ili waweze kuifanya bishara vizuri.

Wamesema tayari wameshapewa samas ya kuhama hapo hivyo nao wanasubiri kupewa mrejesho wa nini serikali inafanya juu ya uboreshaji wa soko hilo.

Kwa upande wa mwenyekiti wa genge hilo la Nyasura Petro Chakoma amesema ameshafika katika soko hilo la manjembe na kujionea hali halisi ilivyo ambapo hali bado ni mbaya katika muonekano wa soko hilo ikiwa ni pamoja na mazingira ya soko kuwa machafu  ndani na nje ya soko.

Hatua ya kuhamishwa kwa wafanyabiashara inajiri baada ya Diwani wa Kata hiyo Mwamba Mangambo Wasira kusika kupitia radio mazingira fm akisema kuwa ni moja ya ahadi yake kipindi anaomba kura kwa wananchi na kwamba uhamishaji huo si wale tu wanaofanyia biashara zao katika genge la nyasura bali ni kwa wote ambao wanafanyabiasha katika mazingira hatarishi kama vile kandokando ya barabara na maeneo kama hayo ndani ya Halmashauri ya mji wa mji wa Bunda.
  

No comments:

Post a Comment