Walimu 22 wakiwemo wa shule ya msingi na sekondari wilayani Tarime waachishwa kazi. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 5 March 2018

Walimu 22 wakiwemo wa shule ya msingi na sekondari wilayani Tarime waachishwa kazi.WALIMU 22 wakiwemo wa shule za msingi na sekondari wilayani Tarime mkoani Mara, wameachishwa kazi kwa utoro na kujihusisha na uhalifu.

Walimu hao wanadaiwa kutoroka tangu Juni mwaka jana sambamba na mwalimu Samwel Daniel wa Shule ya Msingi Mriba anayetuhumiwa kuwabaka wanafunzi tisa.

Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Tarime, Julias Agutu amesema kuwa, “Tume yetu ya utumishi wa Walimu wilayani Tarime imekuwa ikipokea malalamiko na matatizo ya walimu kutoroka na nidhamu.

Hivyo kuanzia Juni mwaka jana tumefukuza walimu 22.

Wengi tuliowafukuza ni watoro lakini tuna mwalimu Samwel Mariba anayetuhumiwa kuwabaka wanafunzi tisa katika shule ya msingi Mriba na ana kesi hizo mahakamani,” amesema.

No comments:

Post a Comment