MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM Bara, Philipo Mangula amewataka Watanzania kujenga na
kuilinda amani nchini na kushangazwa na viongozi wa dini wanaobariki chuki kuwa
wanamkosea Mungu.
Pia
aliwaonya wanasiasa wanaochochea chuki na kusababisha vurugu na kuwashauri
waache kwa kuwa siasa ni uvumilivu na kuumiliana.
Mangula
alitoa kauli hiyo mjini Musoma alipozungumza na viongozi na wana wana
chama wa CCM kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama mjini humo.
Alisema
kuwa turufu kubwa iliyobaki kwa CCM na watanzania ni amani iliyodumu nchini kwa
miaka dahari na hivyo wakati wote wazungumzie taratibu na kutunza amani ya nchi
ili kue[uka machafuko vurugu na migogoro inayosababishwa na kuchochewa na
wanasiasa.
“Siasa ni
kuvumiliana na uvumilivu ndiyo hujenga umoja.Wanasiasa wanapoleta vurugu
wajue wanaoumia ni watoto na wanawake na hivyo tuache chuki tujenge amani ya
nchi yetu bila kufanya hivyo hatuwezi kupata maendeleo,”alisema Mangula na
kuongeza kuwa;
“Nashangaa
na kushitushwa na viongozi wa dini wanapojiingiza na kubariki chuki, wanamkosea
Mungu.Machafuko yakishatokea hakuna atakayesalimika kwa kusema mimi ni kiongozi
wa dini.”
Alieleza
kuwa kazi ya serikali ni kuwajengea nyumba bali mazingira mazuri wananchi
ili wajijenge na kujifanyia maendeleo.
Makamu
Mwenyekiti huyo wa CCM bara alieleza zaidi kuwa yapo mabadiliko makubwa ya
maedeleo mkoani Mara na yote hayo yanafanyika kwa kuwa nchi ina utulivu kwani
bila amani ni vigumu kupata maendeleo na hivyo amani kwanza taratibu na kanuni
zifuatwe baadaye.
Alisisitiza
wanasiasa kuwa wanapochochea chuki na vurugu wanakuwa na passports (hati
za kusafiria) mikononi na yakichafuka wanaondoka na kuwaonya wana CCM
wasijiingize kwenye migogoro hasa vijana wa CCM wasijiingize humo.
Aidha,
Mangula aliwapongeza wabunge wa CCM mkoani Mara walio karibu na wanaotekeleza
Ilani ya uchaguzi ya CCM na ahadi kwa wananchi na wapiga kura wao.
Awali
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samuel Kiboye Namba Tatu alisema Mangula ni
miongoni mwa viongozi waadilifu waliobaki ndani ya CCM na Tanzania.
Alimpongeza
kwa kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais John Magufuli na kuiwezesha CCM
kurudisha heshima kwa wananchi na akawataka wana CCM kumuombea maisha marefu.
“Nakupongeza
kwa kumsaidia Rais Magufuli na sisi huku chini hatutamvumilia mtu yeyote asiye
na nidhamu wala maadili.Wabunge wa CCM nao wamejitahidi kutekeleza ilani ya
Chama hasa mbunge wa Musoma Mjini jimbo ambalo ni gumu kisiasa,”alisema
Namba Tatu.
Kwa mujibu
wa habari ambazo gazeti hili imezipata Mangula atakuwa na ziara ya siku tatu
katika wilaya za Tarime, Serengeti na Bunda ambako atafanya vikao na viongozi
wa serikali na jumuiya za CCM.
Jumanne na
Jumatano atakuwa Tarime, Alhamisi na Ijumaa atakuwa Serengeti kabla ya
kuhitimisha ziara yake jumapili wilayani Bunda.
No comments:
Post a Comment