Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Bunda amekabidhi vitendea kazi katika kata ya Namuhura-Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 13 March 2018

Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Bunda amekabidhi vitendea kazi katika kata ya Namuhura-Bunda Mara



Ziara ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Ndg Gasper Charles akiambatana na Katiba wa UVCCM Wilaya Ndg Steven E. Shija imeendelea kupamba Katika Jimbo la Mwibara lenye Kata 12 ndani ya Wilaya ya Bunda yenye Majimbo Matatu ya Uchaguzi na Kata 33.

Siku ya leo Ziara imeendelea Katika Kata ya Namuhura na Iramba ambapo Vikao vya Baraza Maalumu vilikaa na Kujadili Changamoto mbalimbali zinazowakabili Vijana pia Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utekelezaji alikabidhi Muhuri, Kanuni na Daftari maalumu kwa ajili ya kuandikia Kumbukumbu za Jumuiya
Katika Kata ya Namuhura baada ya Kikao cha Baraza Maalumu la Kata Viongozi wa Kata walieleza Changamoto ya Elimu na Huduma ya Afya, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya na Katibu waliongozana na Viongozi hao kwenda kujiridhisha.

Baada ya Kufika Katika Shule ya Msingi Namuhura Stoo Uongozi wa UVCCM Wilaya ulibaini upungufu wa Madarasa na Nyumba za Waalimu na uongozi ukawaomba Waalimu na Kamati ya Shule kuratibu zoezi la Kupata Vifaa vya Ujenzi, na UVCCM ipo tayari kuweka Kambi Maalumu kusaidia Ujenzi huo mpaka Ukamilike.

"UVCCM tunalojukumu la Kusimamia Elimu za Vijana wetu, mkiratibu zoezi la kupata Vifaa vya Ujenzi tutaleta Vijana hapa tusaidiane kujenga Usiku na Mchana ili kupunguza changamoto hizi" alisema Shija

"Tunaomba Mkuu wa Shule na Kamati ya Shule muhakikishe Jengo hili bovu mnalibomoa lisijeleta athari kama tulivyosikia Nyamang'uta, Katibu kaishasema vyema, UVCCM tupo tayari kuhakikisha mambo yanakaa sawa maana ndiyo utekelezaji wa Ilani ya CCM" alisema Gasper

Pamoja na yote Vijana waliojiunga Kwenye Vikundi waliendelea kuhimizwa kuvifanya Vikundi hivyo kuwa na tija kwa Vijana, pia Vijana ambao hawajajiunga kwenye Vikundi wahakikishe wanajiunga kwenye Vikundi ili Fedha zinazohangaikiwa na UVCCM zinazotoka Halmashauri ziweze kuwanufaisha
Mwisho, Vijana walihimizwa kujikita kwenye Uzalishaji ili kuondokana na Utegemezi, pia Vikundi Vilivyokopeshwa vilikumbushwa kurejesha Fedha walizokopeshwa ili kuondoa dhana ya Vikundi vya Vijana kutokopesheka
Imetolewa na :
Ndg S.E.Shija
Katibu wa UVCCM Wilaya
Bunda,Mara

No comments:

Post a Comment