Tanzania, Burundi na Rwanda
zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani katika
orodha ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa kuhusu viwango vya furaha duniani.
Burundi ndilo taifa ambalo wakazi
wake hawana furaha zaidi duniani katika nafasi ya 156 ambapo imechukua nafasi
hiyo kutoka kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) iliyokuwa inashikilia nafasi
hiyo mwaka jana.
CAR ndiyo inayoifuata Burundi katika
orodha ya mwaka huu.
Tanzania imeshika nafasi ya 153 sawa
na mwaka jana huku Rwanda pia ikishikilia nafasi ya 151 sawa na mwaka jana kati
ya mataifa 156.
Orodha ya mwaka jana hata hivyo
ilishirikisha mataifa 155.
Taifa linaloongoza kwa furaha
duniani mwaka huu ni Finland, kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UN ambapo nchi hiyo
imechukua nafasi hiyo kutoka kwa Norway.
Ripoti hiyo huangazia furaha waliyo
nayo watu wa taifa furahi na chanzo cha furaha hiyo.
Mataifa ya Ulaya Kaskazini
yanashikilia nafasi tano za juu kwa kuwa na viwango vya juu vya raia
walioridhika, huku nchi zilizoathiriwa na vita vya muda mrefu pamoja na nchi
kadha za Afrika Kusini mwa Sahara zikiendelea kwa mara nyingine kushikilia
nafasi tano za chini.
Burundi, taifa ambalo raia hawana
furaha zaidi, lilitumbukia kwenye mzozo wa kisiasa baada ya Rais Pierre
Nkurunziza kuamua kuwania tena urais kwa muhula wa tatu mwaka 2015.
Mwaka huo
kulitokea pia jaribio la mapinduzi ya serikali.
TAZAMA HAPO CHINI
Nchi zenye watu walio na furaha
Duniani
|
Nchi zenye watu wasio na furaha
Duniani
|
1. Finland
|
147. Malawi
|
2. Norway
|
148. Haiti
|
3. Denmark
|
149. Liberia
|
4. Iceland
|
150. Syria
|
5. Switzerland
|
151. Rwanda
|
6. Netherlands
|
152. Yemen
|
7. Canada
|
153. Tanzania
|
8. New Zealand
|
154. South Sudan
|
9. Sweden
|
155. Central African Republic
|
10. Australia
|
156. Burundi
|
No comments:
Post a Comment