Wakazi wa vijiji vinavyopakana
na hifadhi ya taifa ya Serengeti
wamehamasishwa kutafuta suluhu ya pamoja ili kuzuia wanyama pori waharibifu
ambao wamekuwa changamoto katika vijiji vyao.
Akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Tingirima kilichopo kata ya Mugeta
wilayani Bunda mwakilishi kutoka kampuni
ya wawekezaji ya Grumet Fund David Mwakipesile
ambao pia ni waratibu wa elimu hiyo
amesema kuwa kama kampuni wameamua kutoa elimu hiyo kwa vijiji vyote vya
wilaya ya Bunda hasa vijiji vya Mugeta, kyandege, sarakwa,mariwanda,kihumbu,hunyari,
nyamatoke,bukhore, kunzugu na kumaliza na kijiji cha balili kwa kusudi la
kuweka mikakati ya pamoja ya kuzuia wanyama pori waharibifu.
Mwakipesile amewaambia
wanaTingirima kuwa wao kama kampuni
baada ya kuona tatizo la wanyama
waharibifu kama tatizo la kitaifa wameamua kuanzisha kikosi maalum
kinachosaidia kufukuza wanyama hao na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kikosi hicho .
Naye afisa Wanyama pori wilaya ya Bunda Marwa Kitende
amesema kuwa lengo la serikali siyo
kulipa fidia ama kifuta machozi kwa
wananchi bali lengo lao ni kuhakikisha
wanazuia wanyama hao kabla hawajafanya uharibifu.
No comments:
Post a Comment