Update ya tukio la kifo cha aliyekuwa mmiliki wa mabasi ya super sami-Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 15 March 2018

Update ya tukio la kifo cha aliyekuwa mmiliki wa mabasi ya super sami-Bunda MaraKamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafary Mohammed amesema kuwa tayari jeshi la polisi linawashikiria watu wanne kufuatia tukio la kifo cha aliyekuwa mmiliki wa wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah.

Mwili wa Samson Josiah umekukutwa mto Ndabaka eneo la Bunda –Lamadi ukiwa umewekwa kwenye mifuko.

Radio Mazingira fm imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafary Mohammed kwanjia ya simu ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo ambapo amesema hadi sasa wanawashikiria watu wane na kwamba bado jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa tukio hilo.

Aidha Jafary amesema chanzo cha kifo cha mmiliki wa mabasi hayo bado hakijajulikana lakini upelelezi unaendelea ili kubaini nini kisa hasa cha tukio hilo.

No comments:

Post a Comment