NSAJIGWA; Kuna Wachezaji Walikuwa Mizigo leo Yanga Vs Stand United - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 12 March 2018

NSAJIGWA; Kuna Wachezaji Walikuwa Mizigo leo Yanga Vs Stand United

                    
                         

MABINGWA watetezi, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibamiza Stand United mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Ushindi huo unaifanya ya kocha George Lwandamina anayesaidiwa na Mzambia mwenzake, Noel Mwandila na wazalendo Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali kufikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 21. 

Yanga sasa wanalingana kwa pointi na vinara wa muda mrefu msimu huu, Simba SC ingawa mabingwa hao watetezi wamecheza mechi moja zaidi. 

Katika mchezo wa leo, mabao ya Yanga SC yamefungwa na beki wa Stand United, Ally Ally aliyejifunga, kiungo Ibrahim Ajib na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa.

No comments:

Post a Comment