Barabara yapewa jina la Mbunge Ester Bulaya-Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 12 March 2018

Barabara yapewa jina la Mbunge Ester Bulaya-Bunda Mara



Wakazi wa  mtaa wa Bigutu katika halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara wameipa jina la mbunge wa Bunda mjini barabara yenye urefu wa kilomita moja pointi tisa baada ya jitihada za mbunge huyo za kuwafikishia huduma ya barabara ambayo wameikosa kwa muda mrefu.

Wakizungumza katika mkutano uliofanyika siku ya ijumaa ikiwa ni sehemu ya ziara ya mbunge huyo ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia mfuko wa jimbo wananchi hao wamesema kuwa wanampongeza mbunge huyo kwa kuwafikishia barabara ambayo itachochea maendeleo mtaani hapo.

Wananchi hao wamesema kuwa wameamua kuipa jina la ester  bulaya barabara hiyo ikiwa ni kumbumbu na jitihada za mbunge huyo za kuwaletea maendeleo katika eneo lao kwani wameonekana kuwa wamesahaulika kwa mda mrefu.

Naye mbunge wa jimbo la Bunda mjini Ester buyala amesema kuwa uwepo wa barabara hiyo  utawasaidia wakazi wa eneo hilo kutatua changamoto ndogondogo zinazowakabiri.

No comments:

Post a Comment