Tangu kuanzishwa kwa jukwaa hili mwaka 2005 limesaidia wanawake wengi katika kuhakikisha wanazifikia ndoto zao
Na Adelinus Banenwa
Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge amezielekeza halmashauri za wilaya ya Bunda kuandaa program maalumu kwa ajili ya kutoa elimu ya mikopo kwa akina mama wajasiriamali ambao wanajiunga katika vikundi ili kupunguza changamoto za mikopo kwa akina mama hao
Dc kaminyoke ametoa maelekezo hay oleo may 8 2025 katika uzinduzi wa chemba ya wanawake wajasiriamali wilaya ya Bunda chini ya TANZANIA WOMEN CHEMBER OF COMARCE.

Baadhi ya wanachama na wanufaika wa chemba hiyo wamesema kuna fursa mbalimbali kwa wanawake kujiunga na umoja huo kutokana na kukutanishwa na wataalamu mbalimbali pamoja na taasisi za serikali zinazowapatia elimu ili kukabiliana na changamoto za kibiashara katika ujasiriamali wao
Aidha wametoa wito kwa wanawake wengine kutoogopa kujiunga na jukwaa hili kwa kuwa wapo walioanza pasipo kuwa na uelewa lakini hadi hivi sasa wametengeneza mtandao mkubwa wa biashara.

Kwa upande wake mkurugenzi wa jukwaa hili la TWCC Maria Isidory amesema tangu kuanzishwa kwa jukwaa hili mwaka 2005 limesaidia wanawake wengi katika kuhakikisha wanazifikia ndoto zao katika kuwasaidia elimu ya biashara, mitaji na kuwakutanisha na wataalamu pamoja na taasisi za serikali kama vile TRA, SIDO miongoni mwa taasisi zingine
No comments:
Post a Comment