Katika utetezi wake mshitakiwa aliiomba mahakama imuachie huru kutokana na yeye kuwa ni mjane na ana watoto watano wanamtegemea.
Na Adelinus Banenwa
Mahakama ya wilaya ya Bunda imemuhukumu kifungo cha masharti (condition discharge) cha kutokutenda kosa lolote ndani ya miezi sita Neema Msimu John(28), Mkazi wa mtaa wa Mapinduzi kwa kosa la ukatali dhidi ya mtoto wake mwenye umri wa miaka minne kwa kumchoma moto kwenye mkono wake wa kushoto kwa kosa la kujisaidia hovyo.
Hukumu hiyoimetolewa na Hakimu mkazi Mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Bunda, Betron Sokanya, baada ya mshitakiwa kukiri kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume na kifungu Cha 169A(1) na (2) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.
Katika utetezi wake mshitakiwa aliiomba mahakama imuachie huru kutokana na yeye kuwa ni mjane na ana watoto watano wanamtegemea huku mmoja wapo akiwa ananyonya.

Awali kabla ya hukumu kutolewa, mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri Aristariko Msongelo ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwefundisho kwa jamii kuacha tabia ya ukatili dhidi ya watoto.
‘‘Naomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa jamii kuacha tabia ya ukatili dhidi ya watoto’’. Aristariko Msongelo mwendesha mashitaka wa Jamhuri Wilaya ya Bunda.
Aidha Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya Bunda Florence Debogo awewaasa wazazi kutotumia adhabu kali kwa watoto na badala yake watumie adhabu mbadala kama kumnyima mtoto kuangalia television na kuto kwenda kucheza ili kupunguza wimbi la ukatili kwa watoto.
No comments:
Post a Comment