Thursday, 8 May 2025

Upatikanaji wa samaki wengi waathiri biashara ya nyama Bunda

 

Wateja wamepungua kwa kasi katika siku za hivi karibuni kutokana na watu wengi kuelekeza nguvu zao katika kununua samaki

Na Thomas Masalu

Imeelezwa kuwa katika mji wa Bunda, upatikanaji mkubwa wa samaki kwa sasa umeanza kuathiri kwa kiasi kikubwa biashara ya nyama ya ng’ombe, hali inayowatia hofu baadhi ya wafanyabiashara wa nyama hiyo.

Wafanyabiashara hao wamesema kuwa wateja wamepungua kwa kasi katika siku za hivi karibuni kutokana na watu wengi kuelekeza nguvu zao katika kununua samaki ambao wanapatikana kwa wingi sokoni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti leo Mei 7, 2025, na redio Mazingira FM katika eneo la genge la jioni, wafanyabiashara hao wameeleza kuwa tofauti ya bei kati ya samaki na nyama ya ng’ombe imechangia kushuka kwa mzunguko wa biashara yao.

Wafanyabiashara hao wamesema kuwa licha ya changamoto hiyo, bado wana matumaini kuwa hali itabadilika pindi upatikanaji wa samaki utakapopungua.

Sauti ya Wafanyabiashara

No comments:

Post a Comment