Friday, 16 May 2025

wanafunzi Migungani Sekondari watembelea Mazingira fm

 




Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne kutoka Shule ya Sekondari Migungani wakiwa kwenye chumba cha kurushia matangazo radio Mazingira Fm

Wamesema kuwa ziara hiyo imewapanua uelewa wao kuhusu namna vyombo vya habari vinavyofanya kazi.

Na Taro Michael

Wanafunzi wa kidato cha nne kutoka Shule ya Sekondari Migungani, iliyopo wilayani Bunda, mkoani Mara, wamefanya ziara ya kielimu katika Redio Mazingira FM kwa lengo la kujifunza kwa vitendo kuhusu mawasiliano na utangazaji wa redio.

Ziara hiyo ni sehemu ya mtaala wa elimu unaolenga kuwajengea wanafunzi uelewa wa kina kupitia mafunzo ya vitendo, hasa katika masomo ya lugha, uraia, na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne kutoka Shule ya Sekondari Migungani wakiwa nje ya ofiza za radio Mazingira Fm

Wanafunzi hao takribani 20 walipata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali vya utangazaji, kujionea kwa macho namna vipindi vinavyoandaliwa, kurekodiwa na hatimaye kurushwa hewani. Pia walijifunza mbinu za ukusanyaji wa habari, uandishi wa taarifa na uhariri wa vipindi vya redio.

Aidha baadhi ya wanafunzi walieleza kufurahishwa na kile walichojifunza. Wamesema kuwa ziara hiyo imewapanua uelewa wao kuhusu namna vyombo vya habari vinavyofanya kazi na kuwaongezea ari ya kuchangia maendeleo kupitia fani ya mawasiliano.

sauti za wanafunzi

No comments:

Post a Comment