Kobe ni wanyama kama walivyo wanyamapori wengine na wanalindwa kisheria tuwatunze.
Na Catherine Msafiri,
Jamii imetakiwa kuendelea kuwatunza na kuwalinda kobe kwaajiri ya manufaa ya vizazi vijavyo kwani ujangili dhidi yao unahatarisha uwepo wa mnyama kobe kwa miaka ijayo.
Hayo yameelezwa na afisa wanyamapori kutoka TAWA kanda ya ziwa ndugu,Lusato Masinde alipofanya mahojiano na radio Mazingira fm kwenye kipindi cha uhifadhi na utalii.
Aidha Masinde ameeleza kuwa binadamu ndie kiumbe hatari zaidi kwa mnyama kobe kutokana na shughuli zao hasa pindi wanapochoma misitu
Pia amebainisha kuwa mnyama kobe anafaida mbalimbali kiuchumi, kiikolojia na kijamii
Hata hivyo ameeleza sifa za mnyama kobe huku akibainisha kuwa kisheria watu wanaweza kuanzisha mashamba ya kufuga kobe isipokuwa tu kwa kuzingatia sheria na taratibu.
No comments:
Post a Comment