Ndege Makebe Karando (31) amuua kwa kumchoma visu aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni muhudumu wa afya katika zahanati ya marambeka Zawadi John Kazi (35) kisha na yeye kujinyonga.
Na Adelinu Banenwa
Vilio na sintofahamu vimeendelea kutawala kwa wakazi wa kijiji cha Marambeka kata ya Ketare halmashauri ya wilaya ya Bunda kufuatia tukio la Ndege Makebe Karando (31) kumuua kwa kumchoma visu aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni muhudumu wa afya katika zahanati ya marambeka Zawadi John Kazi (35) kisha na yeye kujinyonga.
Makebe Karando baba mzazi wa ndege amesema tukio hilo la kijana wake kufanya mauaji kisha na yeye kujinyonga limewaachia majonzi makubwa kutokana na wote waliopoteza maisha alikuwa akiwachukulia kama watoto wake.

Makebe amesema karando alikuwa na wake wawili lakini pia alikuwa na mahusiano na muhudumu huyo wa afya na tayari walishajitambulisha kwake na mara ya mwisho ilipotokea sintofahamu baina yao walimfikia na akawashauli na walimuhakikishia kuwa mgogoro umeisha hadi pale alipopata taarifa za tukio la mtoto wake Ndege kumshambulia Zawadi
Makebe anaeleza kuwa majira ya usiku alipokea taarifa za Zawadi kushambuliwa na Ndege lakini alikuwa hajamuona ndege japo taarifa za ujio wake pale kijijini alikuwa nazo kwa kuwa mtoto wake huyo anaishi maeneo ya Mugumu Serengeti ambako ana mke mwingine

Ameongeza kuwa wakati asubuhi kesho yake wanajiandaa kama nzengo kujikusanya ili waanze kumtafuta ndege na kumtia nguvuni kutokana na tukio alilolifanya ndipo alipopata taarifa kuwa mtoto wake huyo amekutwa shambani akiwa amejinyonga kwenye mti aina ya mkwaju na alpokwenda alishuhudia kweli Ndege amejinyonga
Ngei Mashoka rafiki wa karibu wa ndege ameiambia Mazingira fm kuwa aligundua kuwa rafiki yake amejinyonga baada ya kupigiwa simu kutoka Musoma kutoka kwa rafiki yao mwingine akidai amepokea simu kutoka kwa Ndege akidai anaenda kujiua kwa kujinyonga katika moja ya miti iliyo shambani mwake

Huku rafiki huyo akieleza kuwa maelekezo ya ndege yalikuwa endapo watamkuta ameshakufa wamtumie nauli mke wake aliyeko Mugumu aje kwenye msiba
Hata hivyo baadhi ya viongozi katika kijiji hicho akiwemo diwani wa kata ya Ketare Mramba Simba Nyamkinda na mwenyekiti wa kijiji Ramadhani Lukiko wamekemea tabia za vijana kujichukulia sheria mkononi huku wakitoa wito kuwa endapo kuna sintofahamu kwa watu wenye mahusiano ni vema wakapata suluhu kutoka kwa viongozi
Jeshi la polisi kupitia kwa kamanda wa polisi mkoa wa Para Pius Lutumo limethibitisha kutokea kwa matukio hayo mawili yaani kuuawa kwa Zawadi John na Ndege Makebe kujinyonga kwenye mti kwa kutumia shuka huku chanzo cha tukio hilo kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi baada ya marehemu Zawadi kukataa kuendelea kuwa na mahusiano na Ndege.
Zawadi John Kazi aliyekuwa muhudumu wa afya katika zahanati ya Marambeka inatajwa ameacha watoto wawili huku Ndege Makebe akitajwa kuacha wajane wawili na watoto watano
No comments:
Post a Comment