Jiungeni katika vyama vya ushirika>Waziri Tibeza Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 19 March 2018

Jiungeni katika vyama vya ushirika>Waziri Tibeza Bunda Mara


Imeelezwa kuwa Serikali imetangaza utaratibu mpya utakaotumiwa na wakulima wa kilimo cha pamba kuuza zao  hilo  ifikapo msimu wa pamba mapema mwezi mei mwaka huu.

Utaratibu huo umetolewa na waziri wa kilimo Dr.charles  Tizeba  alipokuwa kwenye ziara yake wilayani Bunda mkoani Mara ya kuangalia maandalizi ya masoko  katika msimu wa kuuza kahawa  na pamba unaotarajiwa kuanza mapema mwezi mei.

Dr.Charles  amewasisitizia wakulima wa zao hilo kufata  utaratibu huo  wakujiunga katika vyama vya ushirika vilivyopo katika maeneo yao  kwani atakaye kiuka hataweza kuuza pamba yake mahali popote na kuongeza kuwa utaratibu huo utatumika nchi nzima.

Akitangaza  kuanza kwa msimu wa zao la pamba  waziri Tizeba amesema kuwa msimu utafunguliwa rasmi mei mosi ambapo amewambia  wakulima  wasiwe na wasiwasi kuhusu bei ambayo itatangazwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment