Jeshi la polisi la kanusha kusababisha ajali ya mwanafunzi wa darasa la pili -Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday, 21 March 2018

Jeshi la polisi la kanusha kusababisha ajali ya mwanafunzi wa darasa la pili -Bunda Mara

Wanafunzi katika shule ya msingi Balili B halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara wameandamana mapema leo  asubuhi hadi zilipo ofisi ya mkurugenzi wa mji baada ya mwenzao kugongwa kwa gari  na kupelekea kifo chake katika kivuko cha watembea kwa miguu kilichopo karibu na shule hiyo.

Tukio hilo la kugongwa kwa gari hadi kufa limempata Mwanafunzi  wa darasa la sita aitwae Julius Nyerere mwenye umri wa miaka 12 na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali teuli ya wilaya ya Bunda DDH.

Mashuhuda wa Tukio hilo wamesema wameshuhudia mwanafunzi huyo akigongwa  kwa gari lenye rangi ya Dark blue ambalo wao wamelihusisha na gari la askari mmoja wa jeshi la polisi.
Kufuatia tukio hilo mwalimu flora isack anaefundisha katika shule hiyo amewalalamikia baadhi ya askari wa jeshi la polisi kumpiga na kumdhalilisha kwa kumvua nguo kwa kile alichoeleza kwamba alihusika kuhamasisha wanafunzi kufunga barabara na kuponda kwa mawe baadhi ya magari ya abiria yaliyokuwa yakipita kuelekea mwanza na musoma.
Kwa upende wa jeshi la polisi wilaya ya Bunda kupitia kwa OCD Jeremia Shila amekiri kutokea kwa tukio hilo la mwanafunzi kugongwa kwa gari hadi kufa ambapo amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na ufuatiliaji wa gari lililohusika na ajili hiyo.
Kwa upande wa madai ya askari wa polisi kuhusishwa na ajali hiyo pamoja na kumshambulia mwali huyo kamanda shila amepinga taarifa hizo na kueleza kuwa tukio hilo limesababishwa na kijana mmoja ambae baadae gari lake lililohusika na ajali limeonekana musoma na wanaendelea kulifuatilia ambapo ameaidi kutoa taarifa kwa umma pindi watakapokamilisha utaratibu wa kumkamata mhusika.

Aidha kuhusu mwalimu flora kushambuliwa amesame hakushambuliwa badala yake alikuwa akiondolewa barabarani kupisha watumiaji wengine wa barabara kuendelea na shughuli zao.

No comments:

Post a Comment