Baraza la madiwani Halmashauri ya mji wa Bunda limepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 25 kwa mwaka wa fedha 2018/2019. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 22 February 2018

Baraza la madiwani Halmashauri ya mji wa Bunda limepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 25 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Imeelezwa kuwa Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara kwa mwaka wa fedha 2017/18, ilikisia kupokea na kutumia jumla ya shilingi bilioni ishirini Milioni mia sita stini, laki tisa na saba Elfu miambili tisini na saba kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato.

Akifungua Mkutano wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo Mwenyekiti Pius Mayaya amesema kwamba mpaka januari mwaka 2018 mtiririko wa fedha kutoka serikali kuu haukuwa mzuri kwa vyanzo vyote vikuu yaani fedha za matumizi ya kawaida na fedha za miradi.

Ambapo amedai kuwa hadi kufikia januari mwaka huu fedha walizopokea ni shilingi bilioni nane milioni miatisa thelathini na tatu laki sita tisini na tano elfu na mia mbili themanini na tisa na senti sitini na sita ambazo sawa na asilimia 43.4% ya bajeti kisiwa.

Aidha kwa mwaka wa fedha 2018/19 halmashauri ya mji huo umepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 25 zitakazotumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Pia Mayaya amesema kwa mwaka huo wa fedha wanatarajia kuajiri watumishi 426 katika idara mbalimbali ikiwa ni sambamba na watumishi 394 wanatarajiwa kupandishwa vyeo.

No comments:

Post a Comment