Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara Wametakiwa kujikita katika Kilimo-Misitu - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 21 February 2018

Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara Wametakiwa kujikita katika Kilimo-Misitu


WAKAZI wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara Wametakiwa kujikita katika Kilimo-Misitu ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi. 

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kikundi  kinachojishughulisha na Uhamasishaji utunzaji Mazingira cha Good Samaritance Bwana Flavian Nyanza.

Amesema Kilimo Misitu ni Kitendo cha Mkulima Kilima Mazao shambani pasipo kuondoa miti. 

Ameeleza kuwa kuna faida nyingi zinazopatikana kupitia kilimo hicho kama upatikanaji wa Rutuba inayotokana na miti inayosaidia uzalishaji wa Mavuno mengi.

Ametaja faida nyingine ni kulinda udongo,pamoja na kupunguza matumizi ya mbole zisizo rafiki zinazoua wadudu rafiki kwa Mazao.

Aidha pamoja na hivyo ametahadharisha wananchi Kuwa siyo kila mti ni rafiki katika shamba hivyo mkulima akitaka kufanya kilimo hicho ni muhimu akaonana na mtaalam wa kilimo alioko karibu na eneo lake.

No comments:

Post a Comment