Zahanati yetu ya Kabasa haina muuguzi anayeishi hapa kijijini>Wananchi Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 24 February 2018

Zahanati yetu ya Kabasa haina muuguzi anayeishi hapa kijijini>Wananchi Bunda Mara




             Hili ni Moja ya jengo katika Zahanati ya Kabasa

Imeelezwa kuwa Zahanati ya  kijiji cha Kabasa kata ya kabasa Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara haina muuguzi anayeishi katika eneo la kazi wote wanaishi mjini Bunda licha ya kuwepo nyumba za kuishi wauguzi katika zahanati hiyo.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na radio Mazingira fm kijijini hapo.

BI NYAMJINJA pamoja na  BI MILKA Wamesema kutokuwepo karibu wauguzi katika eneo la kazi wanapata wakati mugumu wanapokuwa na mgonjwa hasa nyakati za usiku hali ambayo inasababisha kutumia gharama  kubwa ya usafiri kumfikisha mgonjwa katika Hospital ya wilaya kwani kunaumbali kutoka kijijini hapo.

Wamesema kuwa wanashangaa kuona wauguzi wote wa zahanati hiyo kuishi mjini wakati  nyumba zipo za kuishi wao katika zahanati hiyo.

Aidha wamesema kuwa ikifika saa tisa alasiri wauguzi huondoka katika eneo la kazi na kuelekea mjini wanakoishi hivyo kuanzia muda huo hakuna mtu yeyote anayepata huduma katika zahanati hiyo.

Radio mazingira amezungumza na mmoja ya wauguzi kwa masharti ya kutotajwa jina ameseme ni kweli hawaishi hapo kutokana na nyumba hizo kuonekana zinahitilafu hivyo zikilikebishwa wataishi hapo na kwamba suala lakufunga zahanati hiyo na kutoka saa tisa ni kwa mujibu wa sheria sio kwamba wamejitungia wenyewe.

Hata hivyo tulipomtafuta mtendaji wa kata ya Kabasa ELISHA HENRY amesema kuwa kitendo cha wauguzi kusema kuwa nyumba ni mbovu wakati hata hawaishi hapo si la msingi hivyo wao waanze kuishi kama marekebisho yatafanyika bila shida yeyote kwani lipo ndani ya uwezo wao.

Elisha amesema wanahofia kutumia gharama bure kufanya ukarabati kabla ya kuona wauguzi wakiishi hapo hivyo wao wauguzi waanze kuishi ukarabati utafanika bila shida.
        Moja ya nyumba inayotajwa kuwa ndo ya kuishi wauguzi
                     
                           Mazingira ya Zahanati ya kabasa
                     Elisha Henry mtendaji wa kata ya Kabasa



No comments:

Post a Comment