Hii ni wiki ya pili kwa wanafunzi wa shule ya msingi Bunda wakiwa shule baada ya siku 14 kukaa nyumbani - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday, 19 February 2018

Hii ni wiki ya pili kwa wanafunzi wa shule ya msingi Bunda wakiwa shule baada ya siku 14 kukaa nyumbani



Leo ni wiki ya pili kwa wanafunzi wa shule ya msingi Bunda iliyopo Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara kuendelea na masomo kama kawaida baada ya kukamilika kwa ujenzi wa choo ya shule kukamilika.

Akizungumza na Mazingira Fm Afisa elimu Msingi Amos Mtani ambaye aliyekuwa msimamizi katika ujenzi huo amesema kuwa jambo la kwanza wanamshukuru mkurungezi wa mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bunda kwa hatua za haraka alizozichukuwa katika kumaliza changamoto hiyo katika shule ya Bunda ikiwa ni pamoja na siku 14 walizokuwa wamepewa kukamilisha ujenzi huo.
Mtani amesema kwa sasa wanafunzi wanaendelea na masomo yao kama kawaida huku wakipata huduma hiyo ya choo kwa uhakika bila shida yeyote.

Hata hivyo Mtani ametoa rai wa wananchi kuwa mabalozi wema katika kukisimamia choo hicho ili kuendelea kuwa bora na kwa matumizi yanayofaa kwa wanafunzi.

Itakumbuka kuwa Radio Mazingira Fm kupitia kipindi cha Asubuhi leo ndio kipindi cha kwanza kuibuwa suala hili la shule ya Bunda kukoswa choo na kupelekea Wanafunzi kujisaidia mlimani pamoja na Uwanja wa mpira hali ambayo ilipelekea shule hiyo kufungwa takribani siku 14 ili kupisha ujenzi wa choo shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment