Mtanzania adakwa na dawa za kulevya - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 22 February 2018

Mtanzania adakwa na dawa za kulevyaMwanamke raia wa Tanzania Basaida Zena Jaffary amehukumiwa miaka 5 jela baada ya kukamatwa akiwa na mzigo wa dawa za kulevya Kilogram 2.3, aina ya Cocaine na Heroine, zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Milioni 155.

Bi. Zena Jafary ambaye ni mfanyabiashara wa chakula aliwasili nchini Ghana katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka akitumia Ndege ya Shirika la Rwanda Air

Maafisa wa Mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya nchini humo walibaini shehena hiyo ya dawa hizo haramu zilizowekwa katika bahasha mbili

Baada ya kuhojiwa na maafisa hao, Bi. Zena alikiri kumiliki bahasha hizo na kwamba, alipewa Bw. Mandanje Omari raia wa Tanzania na kutakiwa kuzifikisha kwa mtu mmoja anayeishi katika Jiji la Accra.

No comments:

Post a Comment