MECHI za viporo za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara za vigogo, Simba na Yanga zitachezwa katikati ya wiki hii.
Yanga SC watakuwa wenyeji wa Maji Maji ya Songea Jumatano Uwanja wa Uhuru, au Taifa Jumatano wakati Simba SC watakuwa wageni wa Mwadui FC Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga mjini Shinyanga Alhamisi.
Awali mechi kati ya Yanga SC na Maji Maji ilikuwa ichezwe Jumamosi mjini Dar es Salaam na Mwadui FC ufuatie Jumapili mjini Shinyanga.
Lakini mechi hizo zikaahirishwa kwa sababu vigogo hao wa soka nchini walikuwa wanakabiliwa na mechi za kwanza za Raundi ya Kwanza ya michuano ya Afrika.
Yanga ilikuwa inamenyana na Saint Louis Suns United na kuibuka na ushindi wa 1-0 Jumamosi, wakati Jumapili Simba ikashinda 4-0 dhidi ya Gendarmerie Tnare ya Djibouti.
Mechi za jana Mbao ililazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Stand United iliichapa Singida United 1-0 Uwanja wa Namfua, Njombe Mji FC wamelazimishwa sare ya 0-0 na Mbeya City Uwanja wa Saba Saba, Njombe.
Mechi nyingine za jana, Ndanda FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Tanzania Prisons Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Lipuli Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Jioni hii mchezo mmoja wa Ligi Kuu unaendelea Uwanja wa Kaitaba kati ya wenyeji, Kagera Sugar na Azam FC.

No comments:
Post a Comment