Wito
umetolewa kwa wananchi wilayani Bunda Mkoani Mara kujitokeza kwa kwingi kupima
afya kwani ni njia moja wapo ambayo mtu
inamweka huru kama akijuwa maendeleo ya afya yake.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa shughuli za
UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara,
Vitus Gwanko wakati akizungumza na Radio Mazingira fm ofisini kwake wakati
akitolea ufafanuzi yale yaliojiri kwenye baraza la madiwani hivi karibu katika kile
alichokisema katika kikao hicho juu ya serikali kutokuwa na bajeti kwa
sasa ya kuwahudumia wananchi
wa kawaida wanaoishi na virusi vya UKIMWI badala yake
shughuli hiyo imeachiwa mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s).
Gwanko amesema kuwa kwa mwongozo waliyo
nayo sasa halmashauri imeweka bajeti ya
kuwahudumia watumishi wa umma pekee wanaoishi na
VVU ndani ya halmashauri husika na sio watu wa kawaida.
Kwa mujibu wa
Gwanko, halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa sasa haina bajeti ya
kuwahudumia waviu, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya
UKIMWI, upatikanaji wa madawa ya ARV’s na huduma zingine.
No comments:
Post a Comment