Baadhi
ya raia wa Uturuki wanaoishi nchini, wametua kwenye Uwanja wa Taifa kuisapoti
Simba iliyokuwa ikiivaa Gendamarie ya Djibouti.
Simba
ilikuwa ikiivaa timu hiyo katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho
Afrika na kushinda kwa mabao 4-0.
Mashabiki
hao wakiwa na bendera ya nchi yao, muda wote walikuwa wakiishangilia Simba kwa
nguvu.
Hivi
karibuni, Simba walitembelea ubalozi wa Uturuki nchini kwa mwaliko wa balozi na
kupata chakula cha usiku, pamoja.
Mabao
ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Said Ndemla, John Bocco aliyepiga
mawili na Emmanuel Okwi aliyepiga msumari wa mwisho.
No comments:
Post a Comment