JPM awaalika wawekezaji nchini - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday 11 February 2018

JPM awaalika wawekezaji nchini

RAIS John Magufuli amewahakikishia mabalozi wa kimataifa na mashirika yaliyopo nchini kuwa serikali inaendeleza juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji huku akiwaomba kuwakaribisha wawekezaji walioko katika nchi zao kuja kuwekeza.
Aidha, amesema mwaka huu amedhamiria kuendelea kuboresha mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu pamoja na kuboresha miundombinu ya reli, barabara na pia nishati ya umeme kuchochea uwekezaji wa viwanda.
“Watu wanaosema hatuwapendi nyie sekta binafsi wapuuzeni, mimi nawaambia kuwa tunawapenda kwani nyie ni watu muhimu sana katika maendeleo ya nchi yetu, tutaendelea kushirikiana nao kuondoa rushwa na kuwaboreshea mazingira, hivyo muwakaribishe wananchi wenu waje kuwekeza,” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alisema hayo juzi jioni Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na viongozi hao katika hafla ya kuukaribisha mwaka, na kueleza serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji wa ndani na wa nje.
“Mbali na kushughulikia wizi, ukwepaji kodi tumeendelea kushughulikia changamoto zinazokwamisha maendeleo ya nchi, tatizo jingine kubwa ni la kukosekana kwa miundombinu imara ya usafiri na nishati ya umeme,” alisema.
Alisema anafahamu kuwa gharama za usafirishaji pia ni kubwa kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya usafiri, hivyo serikali inaendelea kuimarisha ambapo sasa sehemu kubwa ya nchi ina barabara za lami na pia kuanza ujenzi wa reli ya kisasa itakayotumia umeme reli ambayo itaungana na reli za kwenda Burundi na Rwanda “Tumeanza kuboresha huduma mbalimbali hususani zile zinazogusa wananchi wetu kama vile afya, elimu, maji jambo ambalo limetufanya kuongoza kwa nchi za jumuia ya kusini mwa bara la Afrika,” alisema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment